Posted By Posted On

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA,

Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao mawili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tofauti, akiwa hajafikisha umri wa miaka 18. Fati kwasasa ana umri wa miaka 17 akiwa tayari ameshafiti ndani ya kikosi cha Barcelona akicheza pamoja na Lionel Messi. Kinda huyo alifunga bao katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ferencvaros usiku wa kuamkia jana. Akizungumza baada ya kufunga bao, Fati anajivunia kucheza pamoja na Messi huku akiendelea kujifunza mambo mengi kupitia mkali huyo. “Messi ni Messi, ana uwezo wa kufunga mabao yoyote, muda wote, kila mtu ana furaha kuwa na aina ya mchezaji huyu, hata mimi najifunza mengi kupitia yeye,” alisema Fati. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Messi kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 27, Philippe Coutinho dakika ya 52, lingine likiwekwa kimiani na Pedri dakika ya 82 na Ousmane Dembele dakika ya 89, bao la kufutia machozi la Ferencvaros lilifungwa na Iroh Kharatin dakika ya 70 pia kwa mkwaju wa penalti.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *