Posted By Posted On

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

New York, Marekani

HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu bifu la muda mrefu (sasa limekwisha) kati ya malejendari wa muziki huo, Jay-Z na Nas.

Sasa, Jay-Z akihojiwa hivi karibuni, alisema mama yake aliwahi kumpigia simu enzi hizo na kumwambia aombe radhi. Kwanini?

Ilikuwa ni baada ya mkali huyo kuachia wimbo wa kumkashifu Nas uitwao ‘Ether’, ambao ndani yake anasikika akitamba kuwahi kuchepuka na mpenzi wa Nas, Carmen Bryan.

Huku Jay-Z akidhani ni dongo la maana kwa mpinzani wake, ‘bi mkubwa’ alikasirika, akimwambia aombe radhi kwa sababu amedhalilisha wanawake wote duniani.

Akisimulia hilo la kupokea simu ya mama yake, rapa huyo alisema: “Mama aliniambia ‘mwanangu umeenda mbali sana’. Nikakiri na kuahidi kumaliza tatizo. Lakini sikufanya kukera wanawake wengine, akili yangu ilikuwa kumkera Nast u.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *