Posted By Posted On

MABOSI wa Msimbazi, wameanza maandalizi ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza mwezi ujao na kwa hatua ya awali imesha…

MABOSI wa Msimbazi, wameanza maandalizi ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza mwezi ujao na kwa hatua ya awali imeshapeleka majina ya viwanja vyake itakavyotumia sambamba na uzi watakaovaa msimu huu, huku ikipanga kupeleka majina 25 tu ya kikosi chake kwa mechi zao za awali.

Katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa, Simba imeshapeleka sampo aina tatu za jezi na soksi zenye rangi nyekundu, nyeupe na kijivu ambazo watazitumia katika michuano hiyo na viwanja viwili, Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mechi za ule wa Mo Simba Arena kwa mazoezi yao.

Mabosi wa CAF wanatarajia kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya ukaguzi wa viwanja hivyo, kabla ya Simba kutumia usajili wao wa wachezaji 25 kati ya 28 waliopo sasa kikosini, ikiwa na maana watatu waliosalia watapigwa panga na kazi ikiachwa mikononi mwa Kocha Sven Vandenbroeck.

Taarifa kutoka ndani ya Simba na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi aliyeomba kuhifadhiwa jina ni kwamba kocha Sven ameachiwa msala wa kuchagua wachezaji anaotaka kuwepo kwenye kikosi cha CAF, lakini mipango yao ni kupeleka 25 ili nafasi tano za mwisho zitumike kuleta majembe ya hatari kama timu itasonga mbele.

“Tunaweza kupeleka majina hayo ya 25 na kuacha nafasi tano wazi ili kama ikitokea tukafanya vizuri na kufika hatua ya makundi kuongeza wachezaji katika usajili mdogo wa CAF kama kikosi chetu kitakuwa na mahitaji ya lazima kufanya hivyo,” kilisema chanzo hicho.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *