Posted By Posted On

WACHEZAJI YANGA WAPEWA NENO, KAZE AFUNGUKA

Msomaji wa Yanganews Blog:Kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze anashusha kikosi chake cha kwanza leo dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaze raia wa Burundi amefanya kazi na Yanga kwa takribani wiki moja tangu alipowasili kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic, wakati macho na masikio ya wanachama na mashabiki wa timu hiyo wakiwa na shauku ya kutaka kuona mabadiliko.

Katika mazoezi ya muda mfupu ambao Kaze ameyaongoza tangu alipotua nchini, ni wazi kuwa alitaka kuwa na mfumo ambao utatengeneza nafasi nyingi za kufunga tofauti na ilivyokuwa awali.

Chanzo chetu lilimshuhudia Kaze akifanya kazi ya kuwaleta pamoja wachezaji wote wa kikosi cha kwanza na wale ambao walikuwa hawatumiki ili kuwapa nafasi upya ya kuingia katika kikosi chake cha kwanza.

Kocha huyo alionekana akizungumza kwa muda na Waziri Junior, ambaye hajapata nafasi ya kuichezea Yanga hata mechi moja ya Ligi Kuu Tanzania Bara tangu aliposajiliwa akitokea Mbao FC iliyoshuka daraja.

Mazungumzo ya Kaze pia yaliwahusu Haruna Niyonzima, lakini baada ya mazoezi aliwaita pembeni Deus Kaseke, Lamine Moro na Zawadi Mauya.

Kaze mwenye miaka 40 alisema lengo lake kuzungumza na wachezaji ni kuleta timu pamoja na kila mchezaji kujiona ana umuhimu katika kikosi chake.

“Ni kawaida yangu kusema na wachezaji mawili matatu kabla na baada ya mazoezi, lengo langu nataka kila mchezaji ajione ni sehemu ya timu, asiwepo wakujisikia thamani yake ni ndogo kuliko mwingine, hilo naamini litazaa umoja wenye nguvu ya kufanya vitu kwa pamoja na vikatimia,” alisema.

Katika mchezo wa leo, kocha huyo alisema tayari ana kikosi cha kwanza kwa muda mfupi aliokaa na timu na anaamini kinaweza kufanya vizuri huku akiendelea kufanya maboresho.

“Nimeendelea kuwasoma wachezaji katika mazoezi yanayofanywa kila siku, nimeanza kukiona kikosi cha kwanza, ndiyo maana kabla ya yote nilitamani kila mchezaji ajione ndani ya kikosi ili asiwepo wa kuona majukumu yake si muhimu,” aliongeza

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *