Posted By Posted On

πŸ”΄ D O N E D E A L πŸ”΄ Azam FC tumefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wao chipukizi, Novatus Dismas, kwenda kwa vigogo wa Israel…

πŸ”΄ D O N E D E A L πŸ”΄

Azam FC tumefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wao chipukizi, Novatus Dismas, kwenda kwa vigogo wa Israel, Maccabi Tel-Aviv @maccabitlvfc.

Dismas anajiunga na timu hiyo baada ya Maccabi kuvutiwa na uwezo wake kwa kipindi cha takribani cha mwezi mmoja alichofanya majaribio ndani ya timu hiyo ambayo imekuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Novatus anakuwa mchezaji wa pili kuuzwa na Azam FC msimu hu, baada ya wiki chache zilizopita kumpiga bei mshambuliaji Shaaban Chilunda, aliyejiunga na Mouloudia d’Oujda ya Morocco.

Mchezaji huyo bora chipukizi wa VPL msimu uliopita, amekuzwa kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Azam FC sambamba na Chilunda kabla ya wote kupandishwa timu kubwa kwa nyakati tofauti.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *