Posted By Posted On

Follow @mawele_jr Al Ahly vs Wydad Casablanca Saa 4:00 Usiku. Al Ahly ana faida ya magoli mawili aliyoyapata nchini Morroco ka…

Follow @mawele_jr

Al Ahly vs Wydad Casablanca
Saa 4:00 Usiku.

Al Ahly ana faida ya magoli mawili aliyoyapata nchini Morroco katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Leo yupo katika uwanja wake wa nyumbani Borg El Arab uliopo mjini Cairo, Egypt.

Al Ahly akiwa katika uwanja huu anakuwa kama Mbogo aliejeruhiwa.
Kwa kifupi tu ana asimilia zaidi ya 75% ya ushindi katika mechi zote alizocheza hapo Borg El Arab.

Ili Wydad Casablanca apenye katika hatua hii ya nusu fainali analazamika kupata ushindi wa magoli matatu zaidi, unadhani itakuwa ni rahisi?.

Moja ya ndoto kubwa ya mabwenyenye wa Al Alhy ni kuona wananyakuwa taji la CAF Champions League walilolikosa kwa muda mrefu sasa.

Ukame wa taji hilo kuliwalazimisha kumtimua kazi Martin Lasarte na walipomuajili Rene Weiler hawakudumu nae, wakamtimua pia.

Kwa sasa wana Pitso Mosimame, moja ya makocha bora tulionao barani Afrika katika kizazi hiki.
Mwaka 2015 aliwapa taji la CAF Champions League klabu ya Mamelodi Sundowns “The Brazilians ” na mwaka huu ana jukumu la kuwapa taji hilo wababe hao wa karne katika bara la Afrika.

Nampa Al Ahly asilimia kubwa ya ushindi kama si kusonga mbele katika mchezo wa leo.

Let’s wait and see.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *