Posted By Posted On

ILIVYOKUWA, MECHI YA YANGA DHIDI POLISI TANZANIA

Msomaji wa Yanganews Blog:Bao pekee lililofungwa na kiungo raia wa Congo dakika 70 limetosha kuipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru, dar es Salaam, jana..

Yanga ililazimika kusubiri dakika 70 kupata bao hilo mfungaji akifunga kwa shuti la kubabatiza lililobadilishwa uelekeo na beki wa Polisi na kumshinda kipa Manyika Peter.

Kocha Cedric Kaze akiiongoza kwa mara ya kwanza miamba hiyo, alikuwa na wakati wa kuangalia mpangilio wa kikosi chake alichokifanyia mabadiliko kutoka mechi ya zilizopita.

Awali chini ya kocha Zlatko Krmpotic, mshambuliaji wa Ghana, Michael Sarpong alikuwa akianza pamoja na kiungo Zawadi Mauya, ambaye jana aliansihwa Farid Musa na Yacouba Sogne, ambaye alikuwa akitokea benchi.

Kaze pia alikuwa na imani na kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima, ambaye alikuwa pia na wakati mgumu chini ya kocha Zlatko, lakini naye alikuwa na nafasi katika timu iliyopangwa jana.

Kipindi cha kwanza, Yanga ilionekana kutawala mchezo lakini kocha wao anatakiwa kufanya kazi ya ziada katika kuwaongezea mbinu washambuliaji wake kuwa makini katika kutumia nafasi wanazotengeneza.

Dakika ya 20 Yanga ilifanya shambulizi kali baada ya kushutukia ugumu wa kuipenya ngome ya Polisi, shuti kali la kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ lilipanguliwa na Manyika na mabeki kuuondoa mpira katika hatari.

Mabadiliko ya Kaze ya kumpumzisha Niyonzima na kumwingiza Ditram Nchimbi yaliongeza nguvu katika kikosi cha Yanga, ambacho pia kilimtumia Sarpong badaye kwenye mchezo huo.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *