Posted By Posted On

Kutoka @azamfcofficial Azam FC tumefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wetu chipukizi, Novatus Dismas, kwenda kwa vigogo wa Isr…

Kutoka @azamfcofficial

Azam FC tumefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wetu chipukizi, Novatus Dismas, kwenda kwa vigogo wa Israel, Maccabi Tel-Aviv @maccabitlvfc.

Dismas anajiunga na timu hiyo baada ya Maccabi kuvutiwa na uwezo wake kwa kipindi cha takribani cha mwezi mmoja alichofanya majaribio ndani ya timu hiyo ambayo imekuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Novatus anakuwa mchezaji wa pili kuuzwa na Azam FC msimu hu, baada ya wiki chache zilizopita kumpiga bei mshambuliaji Shaaban Chilunda, aliyejiunga na Mouloudia d’Oujda ya Morocco.

Mchezaji huyo bora chipukizi wa VPL msimu uliopita, amekuzwa kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Azam FC sambamba na Chilunda kabla ya wote kupandishwa timu kubwa kwa nyakati tofauti.

Klabu yetu itaendelea kuthamini na kuendeleza vipaji vya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi chetu na hatutasita kufanikisha ndoto zao za kwenda kucheza nje ya nchi pale mchezaji anapopata timu na taratibu zote zinapofuatwa na timu husika.

Ahsante sana @novadismac_40 kwa historia yako ndani ya Azam FC na tunakutakia kila la kheri kwenye timu yako mpya.

#sokaplaceupdates

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *