Posted By Posted On

Follow @mawele_jr Michael Sarpong. Pengine labda nimemtazama tofauti lakini ninachokiona sasa itakuwa ni ngumu kufanya vizuri …

Follow @mawele_jr

Michael Sarpong.

Pengine labda nimemtazama tofauti lakini ninachokiona sasa itakuwa ni ngumu kufanya vizuri endapo tu Yanga SC itakuwa haitengenezi nafasi nyingi karibu zaidi na mstari wa goli la wapinzani.

Ni hivi, Michael Sarpong ni mzuri kama akiishi ndani ya boksi la wapinzani, akiwa angalau mita 20 mbali na goli hana madhara makubwa.

Kwa mechi hizi takribani 8 nilizomfatilia sijaona akipiga walau mashuti matatu kutokea nje ya boksi ndani ya mechi moja, hii ina maana kuwa huyu ni mshambuliaji ambae anakula vilivyoiva.

Muwekee mpira njiani, auweke mpira wavuni.
Naamini Cedric Kaze atamtengenezea mazingira rafiki zaidi, lakini kwa namna anavyotumika sasa simuoni Michale Sarpong aking’aa ndani ya VPL.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *