Posted By Posted On

#HeadToHeadStats Mechi ya kesho Jumatatu kati yetu na wenyeji Mtibwa Sugar, itakuwa ni ya 23 kukutana kwenye VPL tokea Azam FC t…

#HeadToHeadStats Mechi ya kesho Jumatatu kati yetu na wenyeji Mtibwa Sugar, itakuwa ni ya 23 kukutana kwenye VPL tokea Azam FC tuanze kucheza katika ligi hiyo msimu wa 2008/2009.

Mechi 22 zilizotangulia, Azam FC tumeshinda mara 10, Mtibwa ikishinda nne kati ya hizo huku mechi nane zikiisha kwa sare.

Jumla ya mabao 45 yamefungwa kwenye mechi zote hizo, Azam FC ikiwa kinara wa ufungaji, ikiwa imeziona nyavu za Mtibwa Sugar mara 29 huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa na Wakatamiwa hao mara 16.

#WeAreAzamFC #TimuBoraBidhaaBora #SARAFU #AzamUngaNambariMoja #AzamUkwaju #AzamUbuyu #AzamStrawberry #UhaiDrinkingWater #TradegentsTanzaniaLimited

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *