Posted By Posted On

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU

KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya Dar es Salaam, mwimbaji mkongwe wa Injili, Boni Mwaitege ameweza kuibuka kidedea dhidi na mwenzake, Emmanuel Mgogo.

Mtangazaji anayesimamamia shindano hilo, Diana Sebua alisema lengo la Nani Zaidi ni kukuza tasnia ya muziki huo nchini na kuwaweka waimbaji karibu zaidi na mashabiki wao.

“Katika mashindano yetu ya leo mashindi ni Boniface Mwaitege  aliyepata kura 34 dhidi ya Emmanuel Mgogo aliyepata kura 15, kura zilipigwa kwa njia ya simu na matokeo yakaonyesha hivyo,” alisema mtangazaji huyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *