Posted By Posted On

Follow @mawele_jr FT Simba SC 0-1 Ruvu Shooting Simba SC anapoteza mechi ya pili mfululizo ndani ya Ligi, haya sio matokeo maz…

Follow @mawele_jr

FT Simba SC 0-1 Ruvu Shooting

Simba SC anapoteza mechi ya pili mfululizo ndani ya Ligi, haya sio matokeo mazuri kwa timu ambayo inagombania ubingwa.

Unampongeza zaidi kocha Boniphace Mkwasa.
Kwanza kwa kupata ushindi na pili ni kwa kuweka mbinu nzuri na bora mbele ya mpinzani wake Sven Vandenbroeck.

Ruvu Shooting walikuwa Superb sana hasa kwenye eneo la Midfield, eneo ambalo Simba SC wana aina ya wachezaji ambao Individual wana uwezo wa kuamua jambo ndani ya dakika 90.

Walichofanikiwa Ruvu Shooting ni kuwazuia viungo wa Simba SC kutokuwa Comfortable katika kumiliki na kupokea Mipira.

Kila ambapo kiungo wa Simba alipopata mpira alifika mchezaji wa Ruvu Shooting na kuizuia pasi ya kwanza kutoka mguuni kwa mpinzani.

Kwa namna moja ama nyengine mbinu hii iliwakosesha uhuru mkubwa Simba SC kutengeneza nafasi katika eneo la mwisho.

Striking Force ya Simba ilikuwa Poor sana, sio kweli kwamba kukoseana kwa Meddie Kagere au Chriss Mugalu kumepelekea yote haya.

Ni ubora mkubwa wa wachezaji wa Ruvu Shooting imekuwa ndio sababu kuu iliyowafanya waibuke wababe mbele ya Wapinzani wao.

Pascal Wawa sijui alifikiria nini pale, yalikuwa ni maamuzi mabovu kutaka kumiliki mpira ndani ya box wakati ambao kuna wachezaji wa timu pinzani zaidi ya wawili ambao wanauwinda mpira huohuo.

Njia sahihi ilikuwa ni kuubutua mpira ili utoke kwenye mazingira yale na kuwaruhusu wachezaji wenzake kuanza kujipanga upya.

Kitu kengine wachezaji wa Simba SC wanafanya Slow Build Up, katika muda mwingi hii iliwasaidia Ruvu Shooting kujipanga vizuri na kufanya maamuzi.

#sokaplaceupdate

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *