Manyika Jr atamani kurejea Taifa Stars
NA ZAINAB IDDY
KIPA wa Polisi Tanzania, Manyika Peter ‘Manyika Jr’, amesema anapambana kuhakikisha anakuwa katika kiwango bora ili aweze kurejea Taifa Stars.
Mayika Jr aliwahi kuidakiwa timu ya Simba msimu wa 2014/15 na mara ya mwisho kuitwa Taifa Stars ilikuwa mwaka 2017 ilipocheza na Malawi.
Akizungumza na BINGWA jijini Dar es Salaam, Manyika Jr kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hayupo katika kikosi cha Stars jambo ambalo linalomkosesha raha.
“Mimi kama Mtanzania nina wajibu kwenye timu yangu ya Taifa ili nipate nafasi ya kucheza natakiwa niwe bora wakati wote na kumshawishi kocha wa Stars kuniita.
“Kwa sasa nafanya mazoezi ya timu na binafsi na ninawashirikisha watu mbalimbali walionitangulia katika soka kwa lengo la kupata ujuzi mwingi zaidi,” alisema Manyika Jr.
,
Comments (0)