Posted By Posted On

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA

SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota nchini, Salmin Salim ‘S2kizzy’, amesema mzuka wa kazi umerudi tena hivyo mashabiki wajiandae.

Akizungumza na Papaso la Burudani, s2kizzy ambaye usiku wa kuamkia jana alikesha studio akiwa na Diamond Platnumz, alisema kazi lazima ziendelee hivyo mashabiki watarajie kusikia mikono yake mingine.

“Asante wote kwa upendo  ambao mashabiki wameuonyesha kwa kipindi hiki nilichopata matatizo mimi na wasanii wangu wa Pluto pia namshukuru Rais Magufuli na serikali kwa kuhakikisha tunapata haki, sasa kazi zinaendelea,” alisema s2kizzy.

@@@

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *