Posted By Posted On

Rekodi mbili za kibabe bao la Yanga

NA MWANDISHI WETU, MWANZA

BAO la pili la Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza jana, limeweka rekodi mbili za libabe.

Bao hilo lilifungwa na Waziri Junior katika dakika ya , akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na winga Farid Mussa aliyeingia kipindi cha pili.

Mbali ya kuipa pointi tatu Yanga kutokana na ushindi wa mabao 2-1, bao hilo limeacha rekodi mbili za kipekee kwenye uwanja huo ambazo zote zinamuhusu mfungaji.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Junior alisema kuwa bao hilo limeingia katika rekodi zake kwani amefunga katika mchezo wake wa 60 wa Ligi Kuu Bara.

Mbali ya hilo, alisema kuwa tangu aanze soka, alikuwa hajawahi kumfunga kipa mahiri na mkongwe Juma Kaseja, hivyo amefarijika kuona jana ametimiza ndoto yake.

“Huu ni mchezo wangu wa 60 hivyo nilipania nifunge bao na nashukuru kocha amenipa nafasi na nimefunga. Pia, nimewafunga makipa wengi wakubwa, lakini nilikuwa sijawahi kumfunga Kaseja. Nashukuru nimemfunga, nimefurahi sana kwa hilo,” alisema.

Akilizungumzia zaidi bao hilo la ushindi la Yanga, Junior alisema kuwa tangu akiwa chumbani kwake, alijua atafunga bao na kweli ikawa hivyo, likiwa .

“Tangu nikiwa chumbani, nilimwambia mwenzangu ninayeishi naye chumba kimoja, Said Makapu kuwa leo (jana) nitafunga bao, na nashukuru nimefunga kweli,” alisema.

Aliahidi kuendeleza cheche zake za kucheka na nyavu katika kila mchezo atakaopangwa akiwa na kikosi cha Wanajangwani hao.

Bao la jana la Junior ni la 34 tangu alipoanza kukipiga Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2015, akiwa amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mbao FC iliyoshuka daraja.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *