Posted By Posted On

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST

MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti kundi lake kupitia video yao mpya, Shoti.

Akizungumza na Papaso  la Burudani jana, Suma Toto alisema ngoma hiyo ni miongoni mwa nyimbo ambazo zitakuwa kwenye albamu ya kundi la The Yeamen lenye wasanii wawili, Chanky Bellah na Suma Toto.

“Tumeachia video ya nyimbo yetu ya Shoti ambayo tutaiweka katika albamu itakayotoka siku za usoni naomba wadau wa itazeme kwenye chaneli yetu ya YouTube,” alisema Suma Toto.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *