Hazard arejesha mzuka Madrid
MADRID, HISPANIA. Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema nyota wake Eden Hazard anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha timu yake kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach, leo Jumanne Oktoba 27, 2020.
Hazard amekuwa akikumbana na majeraha ya mara kwa mara tangu atue Santiago Bernabeu akitokea Chelsea 2019 amecheza michezo 22 tu chini ya Zidane msimu uliopita na kufunga bao moja.
"Hazard kuwa nasi ni kwa sababu yupo sawa na hiyo ni taarifa njema kwetu. Tunafuraha kumwona yupo nasi," amesema Zidane.
"Nadhani tutaona vile ambavyo atatumika. Natambua kuwa msimu mrefu hivyo nitahitaji mchango wa kila mmoja, huo ni ukweli na nimekuwa nikilisema hilo," amesema na kuongeza,Read More
Comments (0)