Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga
NA ZAINAB IDDY
NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), amesema hawakuwa dhaifu mbele ya Yanga, licha ya kuchapwa mabao 2-1, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza.
Akizungumza na BINGWA jana, Kaseja alisema ligi bado ndefu na lolote linaweza kutokea, hivyo kutopata alama tatu dhidi ya Yanga, si sababu ya kukata tamaa kwao, kwani wana uwezo wa kufanya vizuri.
“Ndio kwanza tumecheza mechi ya nane katika ligi na kukosa alama nne katika michezo mitano haiwezi kutukatisha tamaa, kwani tuna nafasi ya kusahihisha makosa yetu na tukafanya vizuri kwenye mechi zinazokuja. “Yanga sio timu mbaya na wala KMC si dhaifu mbele ya Yanga, ulikuwa mchezo ngumu kwetu sote, tulipoteza tu umakini na si kosa la mchezaji mmoja mmoja kwa pamoja tutaipambania timu kwenye mechi zijazo,” alisema Kaseja
,
Comments (0)