Posted By Posted On

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY

KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Katwila ameiongoza Ihefu katika mchezo miwili dhidi ya Azam na kupoteza  kwa mabao 2-0 na baadaye kutoka sare ya kutofungana na Namungo  kwenye Uwanja wa Sokoine.

 Akizungumza na BINGWA kwa simu kutoka Mbeya, Katwila, alisema pamoja na Mbeya City kufanya vibaya, lakini hawataidharau, kwani malengo yao ni kuibuka na ushindi.

Katwila alisema wanaendelea na mazoezi makali kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa fiti kwa mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Alisema mchezo huo utakuwa mgumu, kwa sababu wapinzani wao watahitaji pointi tatu baada ya kuanza vibaya msimu huu.

“Katika ligi hakuna mchezo  rahisi, hata kama timu haijashinda mechi zake au haijafanya vyema, ni lazima kujipanga unaweza kujikuta ukafungwa  hivyo ninaheshimu sana wapinzani wetu,”alisema Katwila. Ihefu wanaburuza mkia baada ya kucheza michezo nane, ikishinda mchezo mmoja, sare mmoja, kupoteza sita huku ikiwa na pointi nne.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *