Posted By Posted On

Kaze amuibua Zahera, aionya Simba

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema aina ya mpira unaocheza kwa sasa na tiomu hiyo, Simba wasiwachukulie rahisi, kwani wanaweza kuwanyang’anya taji lao msimu huu.

Kauli ya Zahera imekuja baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni  (KMC),  ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumza na BINGWA jana, Zahera alisema tangu ujio wa kocha mpya Yanga, Mrundi Cedric Kaze, kikosi cha Wanajangwani kimebadilika na kinacheza soka safi.

“Niliwahi kusema kocha Kaze si wa kumchukulia mdhaha najua anaweza kuipa matokeo bora timu na kama Yanga wakimpa anachohitahi watarajie furaha kulingana na aina ya soka la Tanzania lilivyo.

“Mechi mbili tu timu ikiwa chini yake kila mtu ni shuhuda jinsi mpira wa Yanga unavyochezwa kwa sasa, hii inatosha kuwatahadharisha Simba wanaojitamba kuchukua ubingwa wa ligi kwa miaka 20 mfululizo, lakini pia na timu nyingine zenye nia ya kuchukua taji hilo msimu huu,”

Zahera alisema Ligi ya Tanzania ni ngumu, lakini kama hakutakuwa na vitendo vya uonevu ndani na nje ya uwanja  bila shaka katika mbio za ubingwa kazi itakuwa kubwa kwa timu za Azam, Yanga na Simba.

 Zahera kwa sasa ni mshauri wa benchi la ufundi la timu ya Gwambina inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya kupanda daraja.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *