Posted By Posted On

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY

KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa JKT Tanzania na sasa wanaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba.

Mwadui walipata kipigo hicho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, mkoani Shinyanga.

 Akizungumza na BINGWA kwa simu kutoka Shinyanga jana, Adamu alisema  wachezaji walifanya makosa, hivyo anakwenda kuyafanyia  kazi kasoro zote zilizojitokeza ili waweze kupata ushindi mchezo ujao.

Adam alisema kwa sasa nguvu zote wanazielekeza katika maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Simba utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

“Jana (juzi) tumepoteza matokeo hayajanifurahisha  na nimepokea kwa masikitiko makubwa, kwani ukiruhusu zaidi ya magoli matatu lazima ufungwe, hatuna jinsi, hivyo tunaangalia zaidi mchezo na Simba,” alisema Adam.

Mwadui wanashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi tisa, baada ya kucheza michezo tisa, ikishinda michezo mitatu na kupoteza mitano.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *