Ronaldinho naye ana Corona
RIO, Brazil
MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram, akielezea kuhusu maendeleo ya afya yake. “Nimejitenga, nilikuja Belo Horizonte kwa ajili ya kushiriki tukio la kijamii, niliamua kupima na kugundulika nina maambukizi, ninaendelea vizuri nitarudi na kuungana na familia yangu,” aliandika Ronaldinho. Gwiji huyo alikumbwa na mkasa wa kusota jela, baada ya kukutwa na hatia ya kughushi hati ya kusafiria alipoingia Uruguay mapema mwaka huu.
,
Comments (0)