Posted By Posted On

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU

KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya DR Congo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Tshishimbi  ambaye aliitumikia Yanga kwa misimu mitatu mfululizo, alitemwa mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kumaliza mkataba wake.

Hata hivyo, Tshishimbi kujiunga na AS Vita ilifahamika muda mrefu, lakini uongozi wa klabu hiyo ulimtambulisha jana kupitia ukurasa wa mitandao yao.

“Papy Kabamba Tshishimbi, mchezaji wa zamani wa Yanga, amejiunga na AS Vita, tupendane, tuungane pamoja,” ilisema taarifa hiyo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *