Posted By Posted On

Alex Lwambano: Siku za karibuni inaonekana kama Morrison anakamiwa sana na wachezaji wengine, je ana maneno machafu yanayowaudhi…

Alex Lwambano: Siku za karibuni inaonekana kama Morrison anakamiwa sana na wachezaji wengine, je ana maneno machafu yanayowaudhi kwa hiyo wanaamua kutafuta njia ya kumtia adabu?

Amri Kiemba: Kitu ambacho hakipingiki ni kwamba, Morrison ni mchezaji mzuri. Kila defender anahisi anaweza kumkabili na kuweka mbinu nyingine mbadala ambazo nahisi waamuzi wamekuwa hawatoi fursa kwa wachezaji wenye vipaji kutoa burudani kwa mashabiki.”

“Mbinu zisizostahiki zimekuwa zikitumiwa kuwazuia wachezaji ambao wanaweza kuonesha kile ambacho wanacho. Nadhani waamuzi wanajukumu la kuwalinda wachezaji wenye vipaji ili watu wanaolipa pesa wapate burudani.”

“Haiwezekani kila wakati mechi ikawa ‘one touch’ kama mchezaji anashindwa kucheza kiungwana dhidi ya wenzake apewe kadi akapumzike ili mwingine anaekuja kumkaba atumie mbinu ambazo zimeruhusiwa mchezoni.”

“Waamuzi wangekuwa wanafuata sheria ipasavyo basi kuna wachezaji wengi wangepata kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Morrison. Unakuta mtu mmoja anamfanyia rafu Morrison zaidi ya mara tatu hadi sita na anamaliza dakika 90.”

Ukiachana na yote hayo, hakuna aliyeunga mkono tukio lake la kumpiga ngumi Juma Nyoso. Wote kwa pamoja [Luambano na Kiemba] wanasema tukio lile lilistahili adhabu ya kadi nyekundu lakini kama mwamuzi hakuona basi mamlaka zinaweza kumpa adhabu anayostahili.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *