Posted By Posted On

Photos from SokaPlace’s post

TRIPLE C NA SAYANSI ZA TELEKINESIS, WAPI ILIPO MAABARA YA SAIKOLOJIA TUUTAFUTE UKWELI
.
Zipo imani kwamba binadamu anao uwezo wa kusogeza kitu kwa kutumia ubongo wake tu bila kukishika
.
Unaikumbuka stori ya Merlin yule mwanamaajabu kipindi cha King Arthur karne ya sita? Aliyeweza kutengeneza panga la mwana mfalme kwa macho tu bila kishika kifaa, na kusafirisha jiwe juu ya maji na maajabu mengine mengi
.
Sayansi hii inaitwa Telekinesis ama Psychokinesis, na wanasayansi wamethibitisha hilo japo inasemekana mtu anaweza itumia kwa asilimia 0.17 tu
.
Najiuliza tu, yule Triple C, Cleotus Chotta Chama namba 17 mgongoni pale Msimbazi anaweza kuwa anatumia vizuri hii 0.17 ya uwezo wake wa Telekinesis akisaidiana na mguu wake kufanya anayoyafanya uwanjani
.
Nahitaji maabara ya saikolojia nikajaribu kulithibitisha hili vinginevyo nitakuwa kama mlopokaji
.
Psychokinesis sio tu kusogeza vitu kwa ubongo, ila ina human elctro-magnet connection
.
Vijana likisemwa neno connection mnashtuka, ila hii ni connection ya umeme asili uliopo mwilini mwa binadamu, Mtu aliebarikia kutumia Telekinesis vizuri bila ya yeye kujua, anaweza kumfanya mtu mwingine afanye kitu atakavyo yeye
.
Yawezekana Chama hajui pia, ila anayoyafanya na ule mpira na anavyowafanya mabeki na makipa, jinsi kila pasi anayopokea ni kama amaeomba huku kaelekeza kipimo, maana kila pasi kwake ni nzuri, vivyo hivyo akipeleka kwa wengine
.
Kwa kumuona tu ni dhahiri anacheza zaidi na ubongo ndipo mguu unafuata, mambo mengi yeye ni kama anafanya yanakuwa simple, labda Psychokinesis katika ubongo wake inausogeza ule mpira kabla ya miguu yake, ila nahitaji maabara ya saikolojia kuthibitisha hili
.
Hellow Chama, ni wewe ama ni Merlin wa soka la Bongo born in Lusaka? Hellow Chama, najiuliza tu ni wewe ama ni Harry Porter wa soko la Bongo toka mitaa ya msimbazi, Triple C mwenye Telekinesis zake
.
Basi akishika mpira vibandani utawasikia wanasema “ukimfuata kichwa kichwa, utajua hujui” 😂
.
Dah, bahati mbaya hakuna maabara ya kisaikolojia nijaribu kuthibitisha hili, ama labda naota tu, acha nilale tena alafu niamke toka ndotoni, nikiamka nitarudi tena tuongee uhalisia, naona nakuwa chizi sasa

Prepared by @danirito_thomson

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *