Posted By Posted On

Photos from SokaPlace’s post

#Repost from @caamil_88

1910 – Navigation FC
1926 – 1928- Italiano FC
1930 – New Youngs FC
1935 – YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
1948 – hapo ndipo tulipata rangi zetu rasmi za ( KIJANI, NJANO & NYEUSI)
– alama ya mwenge.
– Ramani ya afrika katika NEMBO YA KLABU YETU.

Aidha, kabla ya uhuru chama cha TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION ( TAA ) kilichoanzishwa mnamo 1929 kwa muda mrefu kilikuwa kikisumbuliwa na WAKOLONI, hapo ndipo TAA iliitumia klabu YANGA kwa ajili ya harakati za kupigania uhuru wa nchi yetu. Vikao vya siri na mpango mkakati ulikuwa ukifanywa na waasisi wa nchi hii kupitia mwamvuli wa YANGA.

Mahusiano hayo yaliendelea baada ya kuzaliwa TANU 1954 mpaka kufanikiwa kupata UHURU WETU mnamo tarehe 9 Disemba 1961 chini ya BABA WA TAIFA – HAYATI Mwl. JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Leo hii wadhamini, Viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wa timu iliyoshiriki kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye mikono ya wakoloni ilifanya ziara ya kutembelea nyumbani kwa BABA WA TAIFA na kufanikio kuzuru kaburi lake lililopo kijijini MWITONGO wilaya ya BUTIAMA mkoani MARA.

Mapokezi makubwa ya kihistoria yalifanywa kwa ukarimu mkubwa wa MAMA WA TAIFA LETU – Bibi MARIA NYERERE, mpenzi na mwananchama wa klabu ya YANGA!

Ama hakika mchango wa klabu yetu ya YANGA ya kusaidia kupigania UHURU utabaki katika kumbukumbu za vitabu vya kihistoria vya taifa hili la TANZANIA.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *