Posted By Posted On

🎯 Chama ni Software kwenye mfumo wa Simba, anaamua muda gani timu iende kwa kasi na muda gani itembee taratibu, Chama anamfanya …

🎯 Chama ni Software kwenye mfumo wa Simba, anaamua muda gani timu iende kwa kasi na muda gani itembee taratibu, Chama anamfanya kila mchezaji wa Simba awe bora zaidi.

🎯 Mwadui alikuwa anajiandaa na mtihani wa taifa wa darasa la saba, akaletewa wa kidato Cha 4. Aliulizwa maswali magumu sana, juhudi za kipa na mshika kibendera ndizo zilifanya kipindi Cha kwanza kiwe na goli 1. Kwa kipindi alichopitia Simba, hii ndo namna ya kuamka na kutoa statement kwamba bado wapo vizuri. Alama 3, goli 5 na Clean sheet.

🎯Yanga amechukua alama 3 kwenye uwanja mgumu kwa kucheza kigumu na kikomavu, uchaguzi wa wachezaji ulikuwa wa kiwango bora. Mchezo wa mpira ni mchezo wa maboksi mawili, unajilinda vipi na unashambulia vipi, Biashara hawakuwa makini kwenye nafasi walizopata, Yanga wamewaadhibu. Wananchi hawajafungwa hata mechi moja mpaka Sasa.

🎯 Namungo anazidi kuimarika kadri ligi inavyosonga mbele. Tuweke imani kuwa mpaka kufikia mashindano ya kimataifa atakuwa ametulia. Alama 3 Safi mbele ya Dodoma.

#M9Updates

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *