Posted By Posted On

FT: Simba SC 5-0 Mwadui FC. Follow @mawele_jr Yes!, yalikuwa ni matokeo mazuri kwa Simba SC kushinda mchezo wa leo ili warudis…

FT: Simba SC 5-0 Mwadui FC.

Follow @mawele_jr

Yes!, yalikuwa ni matokeo mazuri kwa Simba SC kushinda mchezo wa leo ili warudishe hali yao ya kujiamini walioipoteza kwenye michezo miwili iliyopita.

Ukiachana na mazoezi ya kuruka koni, kwenda Gym na kufanya mazoezi kutwa nzima ili upate ubora wa mchezo kwa asilimia 100% ndani ya kiwanja inategemea pia ni namna gani huyo mchezaji amejiandaa kiakili.

Kila mchezaji anapaswa kuwa na utimamu mzuri wa kimwili na kiakili, utimamu wa mwili unapatikana kwa kufanya mazoezi ya nguvu na utimamu mzuri wa kiakili unapatikana kwa mchezaji kuwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi kila anaposhuka dimbani.

Simba walikuwa bora sana leo, hawakuwa na kasi kubwa katikati ya uwanja lakini walikuwa na hatari kubwa kila walipofika katika final third.

Clatous Chama katika mechi nzuri kwake na alisababisha vitu vitokee, mara nyingi alikimbia kupita katika ya mlinzi wa kulia wa Mwadui na beki wake wa kati.
Hii ilisaidia kwa namna moja ama nyengine ku unlock defensive pattern ya Mwadui na kutengeneza mianya kwa John Bocco, Luis Miquissone na Mohammed Hussein ambae ali overlap kupitia upande wa kulia.

Mwadui walikuwa wachovu sana, walikaa nyuma na kuwarusu Simba kuwasogelea mara kwa mara.
Kwa bahati mbaya kwao hawakuwa na safu ngumu ya ulinzi na walikutana na Simba ambayo alihitaji matokeo ya ushindi kuliko kitu chochote.

Said Ndemla, yes! baada ya muda mrefu kupita leo alikuwa katika ubora wake, pasi ndefu na fupi zilizofika kwa mlengwa.
Alicheza nyuma ya Mkude kama deep lying midfielder na kumrahisisha kazi Jonas Mkude ambae aliusaka mpira kila kona ya kiwanja.

Nkosi katika ubora tena kwenye eneo la midfield, kwa bahati mbaya matokeo waliyoyapata kwa namna moja ama nyengine yanampunguzia credit kutoka kwa wadau wa soka lakini ndie aliewapa changamoto nzuri midfielders wa Simba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *