Posted By Posted On

: Aliyekuwa Mkurugenzi wa wanachama wa klabu ya Simba Hashim mbaga, anashikiliwa na jeshi la police kituo Cha Oysterbay daresala…

:
Aliyekuwa Mkurugenzi wa wanachama wa klabu ya Simba Hashim mbaga, anashikiliwa na jeshi la police kituo Cha Oysterbay daresalaam kwa tuhuma za kunaswa kwa mawasiliano yake ya mipango mibaya dhidi yawaajili wake wa Zamani Simba SC

Taarifa ambazo zimethibitishwa kituo Cha police Cha Oysterbay nikuwa Mbaga anashikiliwa toka juzi baada yakushtakiwa na maboss zake hao

Kamanda wa police mkoa wa kipolice kinondoni Edward Bukombe amethitisha jana kukamatwa kwa Mbaga huku akigoma kueleza kwa undani tuhuma zinazomkabili

“Nikweli huyo mtu (Mbaga) tunaye kwasasa lakini hatuwezi kueleza kuna mambo tunashugulika naye lakini kwasasa hatuwezi kueleza chochote kwa undani kwakuwa itakuwa Kama kupoteza ushahidi wa uchunguzi ambao tunaufanya”

Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema Mbaga anashikiliwa kwa kunaswa kwa mawasiliano kweye kompyuta yanayodaiwa ilikuwa ni hujuma dhidi ya timu yake hiyo iliyotoka kupoteza mechi mbili mfululizo.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimesema, ” kwenye WhatsApp web yake kwenye laptop hiyo kulikuwa na mawasiliano aliyokuwa akiyafanya yasiyo mazuri mbaya zaidi alikuwa akiyafanya na mtu mmoja wa huku upande wa pili Sasa hapo ndo wameamua kumkata Ili akajieleze” kilisema chanzo kilichokataa kutajwa

Jana mchana, Mbaga alishuhudiwa kwenye chumba kimoja kituoni hapo akichukuliwa maelezo huku baadhi ya ndugu zake pia wakiwa eneo hilo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *