Posted By Posted On

KMC wawafuata Biashara Utd, watamba

NA MWANDISHI WETU

KIKOSI cha timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC FC), leo kinaondoka jijini Mwanza kuelekea mkoani Mara tayari kwa mchezo wa raundi ya 10 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Ofisa Habari na Mahusiano wa KMC FC, Christina Mwagala, alisema kuwa kikosi chao kimefanya maandalizi kabambe kuhakikisha wanashinda kesho.

Alisema kuwa kikosi hicho kinachonolewa na kocha Habibu Kondo, kimejipanga kuhakikisha kinapata ushindi wa ugenini dhidi ya Gwambina ambapo KMC FC iliondoka na ushindi wa mabao matatu kwa bila na hivyo kuiwezesha timu hiyo kufikisha alama 14 hadi sasa na kuwa katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara 2020/2021.

“Pamoja na kwamba mchezo huo utakuwa mgumu, lakini KMC FC imejipanga kuhakikisha kwamba inapata matokeo mazuri, kila kitu ni mipango na utayari, hivyo tupo tayari kukabiliana na mpambano huo kwasababu uwezo tunao, tunakikosi imara ambacho kinaweza kutupatia matokeo sehemu yoyote”.

Hata hivyo katika kikosi hicho, KMC inamajeruhi wawili ambao ni Emanuel Mvuyekule ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya Gwambina pamoja na Abdul Hillary ambaye anasumbuliwa na goti ambapo aliumia katika mazoezi ya timu lakini afya zao zinaendelea vizuri.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *