Posted By Posted On

MIKONO YA jr_farhanjr CHOZI GEREZANI, CHOZI KWA RONALDO Kaskazini Mashariki mwa Hispania una mji mdogo uitwao Jaca ndani ya Ji…

MIKONO YA jr_farhanjr

CHOZI GEREZANI, CHOZI KWA RONALDO

Kaskazini Mashariki mwa Hispania una mji mdogo uitwao Jaca ndani ya Jimbo la Huesca, ndipo hapo alipokulia Mrembo aitwae Georgina Rodriguez kwa Baba Muargentina na Mama Mhispania

Ugumu wa maisha, kulala bila kula, homa bila matibabu sahihi na vurugu za kodi ndizo zilimkuza Binti huyo mdogo pamoja na Dada yake wa pekee Ivana, huku Mama akiwa mlezi mkuu wa familia

Wakati wanakuwa walilazimika kufika mahakamani kusikia hukumu aliyosomewa Baba yao Mzazi Mzee Jorge Rodriguez, aliekuwa muuza Bangi nchini Hispania na madawa mengine mengi ya kulevya

Nyundo zilipigwa na Hakimu Alberto Mayoral, akimwaga mvua ya miaka 10 Jela na kazi ngumu kwa Mzee huyo wa Mabinti wawili, ndipo hapo chozi la Georgina lilianguka kwa mara ya kwanza, hakuwa na tumaini zaidi ya kupambana familia iishi

Akiwa Mdogo akajifunza kucheza mziki baadae akajifunza Umodo, akasafiri mpaka England kwa ajili ya mafunzo hayo, baadae aliporejea Hispania akatua Jijini Madrid kuanza maisha mapya akiwa na jukumu la kuibeba familia

Kumbuku alishaangusha chozi lake la kwanza, alijiapiza hatolia tena maishani mwake Binti huyo, alikuwa busy na biashara kwenye duka la kuuza nguo la Gucci pale Madrid, walikuja matajiri wengi na Mastaa wengi lakini bado hakuna alievutiwa na muuza duka huyo

Lakini si tunaishi kwa kutimiza andiko au sio Mtu wangu?? Basi asubuhi moja ya saa 5:15 Oktoba 18,2016 nyota wa dunia Cristiano Ronaldo alipark gari yake aina ya Bugatti Veyron nje ya duka hilo na kuingia ndani kutungua viwalo kadhaa, ni Binti huyo aliemuuzia Ronaldo

Ronaldo hakumuwaza sana japo inasemekana walitupiana macho kwa dakika kadhaa ila Mtaalamu alivunga siku ya kwanza kwakuwa Mapaparazzi walikuwa wamejaa, ikumbukwe pia mwamba ana pesa ila hapendi skendo magazetini, maisha yake ni private sana

Mara ya pili wakaonana kwenye shughuli ya Dolce Gabanna ndani ya VIP BOX Madrid hapo hapo, ndipo walipata muda wa kuongea na kubadilishana namba na kilichosalia ni historia, Binti huyo aliangusha tena chozi lake kwa mara ya pili baada ya kuvishwa pete ya uchumba Nchini Morroco

Yote yamebaki historia, machozi mara mbili na imara maradufu🙏 MAISHA NI FUMBO

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *