Posted By Posted On

RONALDO ATOKA KARANTINI NA KUPIGA MBILI JUVE IKISHINDA 4-1

Cristiano Ronaldo amerejea kutoka kwenye karantini kufuatia kukutwa na virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19 na kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 wa Juventus dhidi ya wenyeji, Spezia kwenye mchezo wa Serie A jana Uwanja wa Orogel -Dino Manuzzi, Cesena.
Ronaldo aliyekosa mechi nne zilizopita, alifunga dakika ya 59 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza Alvaro Morata na dakika ya 76 kwa penalti dakika ya 14 baada ya Federico Chiesa kuangushwa na Paolo Bartolomei.
Mabao mengine ya Juventus yalifungwa na Alvaro Morata dakika ya 14 na Adrien Rabiot dakika ya 67, wakati bao pekee la Spezia lilifungwa na Tommaso Pobega dakika ya 32 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *