Posted By Posted On

SENZO, MBAGA, KUNA NINI? . Anaandika @shaffihdauda_ . Baada ya kutoka taarifa za aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki …

SENZO, MBAGA, KUNA NINI?
.
Anaandika @shaffihdauda_
.
Baada ya kutoka taarifa za aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki Simba, Hashim Mbaga kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kudhaniwa anawahujumu waajiri wake wa zamani, bado kulikuwa na maswali mengi kuhusu kukamatwa kwake.

Baada ya kufanya utafiti wa kina, kutoka kwa vyanzo kadhaa, hatimaye nimepata chanzo cha kushikiliwa kwakwe na Jeshi la Polisi.

Kuna mawasiliano ya Mbaga na Senzo yamenaswa [WhatsApp] ambapo wawili hao walikuwa wakijadiliana kuhusu Mbaga kwenda Sumbawanga na kuna jambo ambalo alitakiwa kwenda kulitekeleza akiwa huko.

Katika majadiliano yao, Bw. Senzo aliahidi atatoa kiasi cha pesa kwa ajili ya kugharamia safari ya Mbaga (kwa ndege) kwenda Sumbawanga na kurudi Dar.

Kwa mujibu wa majadiliano yao, inaonekana mpango wao haukuwa Sumbawanga pekee, baada ya kurudi Dar Mbaga alitakiwa kuendelea na jambo lao hadi timu itakapotudi Dar na itakapoingia kambini kwa kujiandaa na mechi ya WATANI WA JADI!

Maswali ya kujiuliza:

1. Wawili hawa walikuwa na mpango gani na Simba kule Sumbawanga? Hashim Mbaga kwa sasa sio kiongozi tena wa Simba, Senzo ameshahama Simba yupo Yanga.

2. Je, Senzo alikuwa anamtumia Mbaga kuihujumu Simba kwa sababu waliwahi kufanya kazi pamoja?

3. Kwa nini Senzo analipa gharama za safari ya Mbaga kwenda kwenye mechi ya Simba wakati yeye sasa kwa sasa yupo Yanga?

Haya mambo ya kuhujumiana na kutafuta matokeo nje ya uwanja hayana afya kwenye soka, kila timu itafute na kupata matokeo uwanjani kutokana na maandalizi iliyofanya.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *