Posted By Posted On

Gwambina FC vs Yanga SC. Follow @mawele_jr Hii ni mara ya kwanza timu hizi zinakutana katika michuano ya ligi kuu. Yanga SC wa…

Gwambina FC vs Yanga SC.

Follow @mawele_jr

Hii ni mara ya kwanza timu hizi zinakutana katika michuano ya ligi kuu.
Yanga SC wameonekana kuwa katika kiwango bora na Gwambina bado anaendelea kusuasua.

Gwambina ina mchanganyiko wa vijana wenye vipaji na wachache wenye uzoefu wa kutosha, Yanga SC kwa asilimia kubwa timu yao ni mpya na bado inaendelea kujengeka kidogo kidogo.

Faida waliyonayo Gwambina ni kucheza katika uwanja wao wa nyumbani, na kwa upande wa Yanga SC wana aina ya wachezaji wanaoweza kuamua matokeo.

Yanga SC imefunga magoli 11 msimu huu na wapo katika nafasi ya pili, wameruhusu mawili katika mechi 8.
Hii ina maana wana timu ambayo iko balanced katika maeneo yote ndani ya uwanja.

Gwambina wamefunga magoli 6 na kuruhusu 10 katika mechi 9, wapo katika nafasi ya 14 na timu yao inaonekana kukosa muendelezo wa matokeo mazuri.

Hii ni mechi ambayo Yanga SC analazimika kushinda ili atengeneze Winning Mentality kuelekea Dadi ya Kariakoo.

Kwa upande wa Gwambina hii ni mechi ambayo wanatakiwa kushinda ili wajiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa VPL.

#Sokaplaceupdate

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *