Posted By Posted On

KAZE ANAWABIPU WANANCHI Katika mahojiano ya kocha wa Yanga leo Cedric Kaze kabla ya mchezo dhidi ya Gwambina ameongea kitu flan…

KAZE ANAWABIPU WANANCHI

Katika mahojiano ya kocha wa Yanga leo Cedric Kaze kabla ya mchezo dhidi ya Gwambina ameongea kitu flani cha kitaalamu sana ila nikasikitika maana nilijua hawezi kueleweka na atajuta kuongea.

Kocha ameulizwa mbona katumia wachezaji wengi ambao hawapo kikosi cha kwanza akasema amecheza mechi nne kwa kutumia wachezaji wale wale hivyo wanachoka lazima awe anabadilisha badilisha kila baada ya mechi kadhaa, ni kauli ya kiufundi ila Asingeisema Tanzania hapa angeisema huko Barcelona

Yani hii kauli angetakiwa aitoe baada ya mechi tena akiwa ameshashinda mechi yani Bora angesema wachezaji wote wanaumwa wamelazwa Mloganzila kuliko kuwaweka jukwaani alafu chini timu inateseka wananchi ni ngumu sana kukuelewa

Kama ndio akili zake kwamba anaweza kupanga kikosi chake anachojiskia kwa Tanzania hii Watamuwamba mbona mapema tu

Mwenzake Sven juzi aliyazua kidogo yamtokee puani. Tanzania kocha kazi yako ni kuwafurahisha mashabiki tu hutakiwi kufanya kazi yako kitaalamu hata kidogo, ukileta utaalamu tu utajikuta kwenu asubuhi

Nadhani kupitia mechi hii atajifunza akili za mashabiki waliomkabidhi timu yake nadhani hatarudia tena Alichokifanya leo

Narudia kocha alikuwa sawa kabisa ila sio kwa Tanzania hii huo utaalamu wa kupumzisha miili ya wachezaji unatokea ulaya tu hapa ni ushindi kila mechi

ALL IN ALL ILE OFFSIDE AU ONSIDE?

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *