Posted By Posted On

MABAO YA AJIB, NDEMLA YANA UJUMBE MZITO

MWANDISHI WETU

WAKATI Simba na Yanga wakitarajia kukutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mabao yalifungwa na Ibrahim Ajib na Said Ndemla yamebeba ujumbe mzito.

Wawili hao ambao hawaonekani kupata ya kucheza mara kwa mara katika kikosi hicho cha Simba, wiki iliyopita walifunga mabao mazuri, wakati wakiibuka na ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ajib aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya John Bocco aliweza kufunga bao safi kwa shuti kali, kabla ya Ndemla  kufunga bao nzuri zaidi ambalo lilikuwa la tano kwa timu yake ya Simba.

Mabao hayo yatakuwa ni  ujumbe wa wachezaji hao kwa kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa hawapi nafasi kubwa ya kuanza katika kikosi chake cha  kwanza, lakini kwa wapinzani wao wanakuja.

Kutokana na kiwango kilichooneshwa na wachezaji hao watakuwa wametengeneza ushawishi kwa Vandenbroeck kuendelea kupanga katika kikosi kitakachocheza kesho dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru na baadaye Yanga.

Katika mchezo huo, Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Bocco  na kabla ya ushindi dhidi ya Mwadui walifungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga mkoani Rukwa,kisha kupata kipigo kama hicho kutoka kwa Ruvu Shooting dimba la Uhuru.

Ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui uliiwezesha Simba kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 16, baada ya kucheza michezo nane, wakishinda mitano, sare moja na kufungwa miwili, huku Azam wakiwa kileleni kwa pointi 22, sawa na Yanga, lakini wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *