Posted By Posted On

SAMATTA AISAIDIA FENERBAHCE KUPANDA KILELENI UTURUKI BAADA YA KUICHAPA ANTALYASPOR 2-1

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (kulia) akishangilia na wachezaji wenzake wa Fenerbahce baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Antalyaspor kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki usiku wa jana Uwanja wa Antalya. 
Mabao ya Fenerbahce yalifungwa na Ozan Tufan dakika ya 49 na Diego Perotti kwa penalti dakika ya 80 na la Antalyaspor lilifungwa na Lukas Podolski dakika ya 52, wakati Samatta alimpisha Kemal Ademi dakika ya 74. 
Kwa ushindi huo, Fenerbahce inapanda kileleni ikifikisha pointi 17, moja zaidi ya Antalyaspor baada ya timu zote kucheza mechi saba. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *