Posted By Posted On

Samatta, Cabaye waingia kikosi cha kwanza KMC

NYOTA Mohamed Samatta na Masoud Abdallah kwa mara ya kwanza wameingia katika kikosi cha kwanza cha KMC ambacho kinacheza mchezo wa Ligi Kuu na Biashara Utd leo saa 10:00 katika Uwanja wa Karume, Mara.

Samatta na Cabaye hawajawahi kuanza katika kikosi hiko ambacho kimeshacheza mechi 9 badala yake walikuwa wakiingia kutokea benchi.

Wachezaji hawa wanachukua nafasi ya Kenny Ally na Hassan Kapalata ambao walikuwa wanaanza katika michezo iliyopita.

Cabaye ambaye ameenda katika timu hiyo kwa mkopo akitokea Azam FC, hajawa akipata nafasi mara kwa mara katika kikosi hiko.

Kikosi cha KMC kinachoanza leo ni Juma Kaseja, Israel Mwenda, Ally Ramadhan, Ismail Gambo, Lusajo Mwaikenda,Jean Mugiraneza, Masoud Abdallah, Martin Kigi.

Wengine ni Paul Peter, Mohamed Samatta na Hassan Kabunda huku katika upande wa benchi wakiwa ni Rahim Abdallah, Hassan Kapalata, Kelvin Kijiri, Reliants Lusajo, Kenneth Masumbuko, David Mwasa na Cliff Buyoya.

KMC wanaingia katika mchezo huo wakiwa na morali ya juu baada ya katika mchezo wao uliopita dhidi ya Gwambina kushinda 3-0.,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *