Posted By Posted On

– Klabu ya Yanga SC imemteua Haji Mfikirwa, kuwa Kaimu Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo…CPA Mfikirwa ambaye awali alikuwa Mkuru…

– Klabu ya Yanga SC imemteua Haji Mfikirwa, kuwa Kaimu Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo…CPA Mfikirwa ambaye awali alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Timu hiyo ya Wananvhi, amechukua nafasi ya Wakili, Simon Patrick, ambaye amesimamishwa kwa sababu ya tuhuma za kuihujumu timu.

– Mara Baada ya kuteuliwa, Mfikirwa amesema licha kutojiunga na Klabu hiyo kwa muda mrefu Kama Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, lakini Klabu imemuamini Zaidi na kumpa nafasi ya Kukaimu Ukatibu Mkuu – Ameongeza Kuwa ”Nafasi hii ni ngumu kwasababu hii ni klabu kubwa na ina mashabiki wengi, lakini nipo kwaajili ya kusimamia utendaji na dira ambayo imewekwa na viongozi”.

– Wakati huo huo kwenye Mkutano na Wana Habari, Uongozi wa klabu ya Yanga umelitaka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) litoe majibu dhidi ya kesi zao mbili zilizopo katika ofisi za Shirikisho hilo – Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela amesema wanashangaa kuona kesi zao zikichelewa kutolewa majibu kwa wakati mpaka sasa.

– Kesi ya Kwanza Ni ya Ramadhan Kabwili ambayo pia Yanga waliipeleka hadi PCCB (Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa) na majibu walipewa lakini TFF bado hawajawapa majibu.

– Kesi ya Pili Ni ya aliyekuwa mchezaji wao, Benard Morrison kutopatiwa majibu ya kuwaridhisha.

🗣️ “Kuhusu kesi ya Morrison,sisi tulizungumza wazi kwamba mkataba sio sahihi ni batili, tuliomba tupewe majibu lakini hatujapata mpaka leo.

🗣️ “Wasiwasi wetu ni kwamba 15 Disemba dirisha dogo linafunguliwa hivyo wanaweza kubadilisha mkataba… Tunawaomba TFF waitishe kesi hii mapema kabla ya dirisha dogo kufunguliwa” Amesema Mwakalebela.
#YangaSC #CAS #BernardMorisson #VPLNews
@harunlugoyah

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *