Posted By Posted On

Uongozi wa klabu ya Yanga SC, umemtangaza Hajji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu mpya ambaye anachukua nafasi ya Wakili Simon Pa…

Uongozi wa klabu ya Yanga SC, umemtangaza Hajji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu mpya ambaye anachukua nafasi ya Wakili Simon Patrick ambaye amesimamishwa kazi.

Wakili Simon amesimamishwa kazi siku tatu zilizopita akituhumiwa kuhujumu timu hali iliyopelekea kuundwa Kamati huru kwa ajili ya kuchukunguza suala hilo kabla ya kutolewa hukumu.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela amesema Kamati ya Utendaji inamuamini Hajji ataweza kuipeleka mbele klabu hiyo kutokana na uwezo mkubwa alio nao.

Mwakalebela ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzifanyia kazi kesi zao walizo ziwasilisha ambazo ni ile ya Ramadhani Kabwili, pamoja na mkataba wa Bernard Morrison kwa kuwa wanaelekea katika dirisha dogo la usajili.

Mwakalebela ameongeza kuwa kama suala la Morrison ambalo limefikishwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo ya FIFA (CAS) kama lisipofanyiwa kazi mpaka dirisha la usajili likafunguliwa huenda mkataba ukabadilishwa kwa kuwa muda utapatikana dirisha likiwa wazi kwa sababu Mchezaji huyo amewasilisha mkataba ambao umesainiwa na pande zote katika Mahakama ya usuluhishi ya kimataifa ya michezo CAS kitu ambacho kimewashangaza.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *