Posted By Posted On

*YOUSSOUFA MOUKOKO* Ushawahi kusikia jina Youssoufa Moukoko? Alijiunga na timu ya Borrusia Dortmund ya umri wa chini ya miaka…

*YOUSSOUFA MOUKOKO*

Ushawahi kusikia jina Youssoufa Moukoko?

Alijiunga na timu ya Borrusia Dortmund ya umri wa chini ya miaka 17 akiwa na miaka 12.
Msimu wake wa kwanza alifunga goli 40 na msimu wake wa pili akafunga 50.

Akiwa na miaka 14 akapandishwa kwenye timu ya umri chini ya miaka 19, akafunga goli 34 kwenye mechi 20 za ligi. Msimu huu kwenye mechi 4 amepiga hat trick 4, akifunga goli 13 mpaka Sasa.

Kwa sheria ya ujerumani, kijana chini ya umri wa miaka 16 haruhusiwi kucheza ligi kuu. Leo Novemba 20, Moukoko anatimiza miaka 16, anapata sifa ya moja kwa moja kucheza ligi kuu na tayari Borrusia Dortmund wamejumuisha jina lake kwenye kikosi kitakachocheza na Hertha Berlin wikiendi hii.

Mtambo huu wa magoli unaenda kuungana na Haaland kwenye safu ya ushambuliaji ya Dortmund.

Baada ya kusubiria kwa muda mrefu tutamshuhudia kijana anayesumbua ligi za vijana huko ujerumani.

Rekodi zake ni Kama ifuatavyo;

Borussia Dortmund U-17:

🎯Mechi 56
⚽Magoli 90

Borussia Dortmund U-19:

🎯Mechi 32
⚽Magoli 51

You are Welcome Moukoko 🦅

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *