Posted By Posted On

Follow @mawele_jr Coastal Union vs Simba SC. Coastal Union haina mfululizo wa matokeo mazuri tangu kuanza kwa msimu huu, timu …

Follow @mawele_jr

Coastal Union vs Simba SC.

Coastal Union haina mfululizo wa matokeo mazuri tangu kuanza kwa msimu huu, timu bado ina struggle kupata ushindi na hakuna eneo lolote lililofanya vizuri mpaka sasa.
Wamefungwa magoli 10 na kufunga 7 pekee.

Jinamizi la kuwakosa wachezaji bora waliowapa makali msimu uliopita bado linaendelea kuwatafuna, Coastal Union iliondokewa na wachezaji muhimu katika maeneo yote matatu ( Ulinzi, Kiungo na Ushambuliaji).

Hii kwa namna moja ama nyengine imewaathiri kwa sababu wachezaji wapya waliosajiliwa bado hawajaonyesha kuwa wao ni watu sahihi wa kuziba nafasi zilizoachwa na watangulizi wao.

Kwa siku za karibuni tumeiona Simba SC ikifanya slow build up, wachezaji hawapendi kugongana na ukiwafanyia pressing kwa namna moja ama nyengine unavunja mpango wao wa mechi.

Kama Simba SC itaingia vilevile kama tulivyoiona katika mechi takribani 2 za mwisho inaweza kuwa faida kwa Coastal Union kama tu wachezaji wake wataamua kuteseka kiwanjani.

Wanachotakiwa kukifanya ni kuwa compact kwenye eneo lao na wajitahidi kutofanya makosa ya lazima, wasiwaruhusu wachezaji wa Simba SC kuwa comfortable na mpira katika kufanya maamuzi na wawe na spidi wakati wa kushambulia.

Simba SC Inakutana na timu dhaifu hasa katika eneo la ulinzi, wao wana safu bora ya ushambuliaji ambayo imeshafunga magoli 22 mpaka sasa.

Presha kubwa ya kutaka kuwa katika kilele cha msimamo wa ligi bado inawasukuma wao kutafuta alama 3 zikiwemo hizi za leo.

Nategemea kuona wakipeleka mashambulizi mengi katika lango la wapinzani wao hasa kwa kutumia mipira ya juu kulingana na mazingira ya uwanja ili wapate bao ambalo litawaweka katika mazingira mazuri.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *