Posted By Posted On

FT: Coastal Union 0-7 Simba SC Mechi ambayo Coastal Union walikuwa poor sana, hawakuwa na nidhamu tangu dakika ya kwanza na saf…

FT: Coastal Union 0-7 Simba SC

Mechi ambayo Coastal Union walikuwa poor sana, hawakuwa na nidhamu tangu dakika ya kwanza na safu yao ya ulinzi ilifanya makosa yaliyojirudia.

Yes! goli la kwanza kwa upande lilikuwa ni offside lakini hata hivyo unawalaumu walinzi kwa kucheza zaidi na filimbi ya refa.

Kosa kubwa lilikuwa ni kumuacha John Bocco apokee mpira akiwa huru na kukaa nao karibu sekunde 5 kabla ya kuupeleka mpira kwa Hassan Dilunga.

Unaweza kusema Simba SC walikuwa bora lakini pia walikutana na Coastal Union iliokuwa dhaifu kuzidi maelezo.

Juma Mgunda alichelewa kung’amua mapema ile approach ya Simba SC ya kutumia mipira mirefu.

Wakati ambao Simba SC wanaumiliki mpira walinzi wao wa pembeni walisimama nyuma ya walinzi wa pembeni wa Coastal Union.

Mpira mrefu kutokea nyuma iliwapa wakati mzuri zaidi Simba SC wa kuwashambulia wapinzani wao kwa sababu tayari walishavuka karibu mistari miwili ya ulinzi.

Sijaona ubora wowote wa Coastal Union katika mchezo wa leo, kuna muda walijaribu kugeza mchezo wa Simba SC ( Possession Football ) na wakajikuta wakiwa katika wakati mgumu mara dufu.

Simba walikuwa quick sana kila walipourudisha mpira katika himaya yao na ile slow build up tuliwaona nayo katika michezo michache ya nyuma.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *