Posted By Posted On

Klabu ya FC Platinum ambao ndio Mabingwa wa Zimbabwe 2019/20 wamemfuta kazi kocha wao mkuu Hendrikus Pieter De Jongh raia wa Uho…

Klabu ya FC Platinum ambao ndio Mabingwa wa Zimbabwe 2019/20 wamemfuta kazi kocha wao mkuu Hendrikus Pieter De Jongh raia wa Uholanzi baada ya kukosa sifa za kuiongoza timu hiyo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mujibu wa CAF.

Hendrikus Pieter De Jongh ana leseni A ya ukocha kutoka UEFA lakini ili uiongoze klabu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lazima awe na leseni & vibali kutoka CAF na kocha ambaye alikuwa anafundisha soka nje ya Afrika anatakiwa awe na Pro License ili aweze kukaa kwenye benchi kwa timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *