Posted By Posted On

#Repost:@hamisi_kigwangalla Nilikutanishwa na Mohammed Dewji na baba yake, Mzee GMD. Kipindi hicho tuki-supply MeTL marobota ya…

#Repost:@hamisi_kigwangalla

Nilikutanishwa na Mohammed Dewji na baba yake, Mzee GMD. Kipindi hicho tuki-supply MeTL marobota ya pamba kutoka kiwandani kwetu. Alikuwa Mbunge wa Singida Mjini na mimi nikiwa nafanyia kazi ndoto zangu za kuingia bungeni. Kuanzia hapo tulikutana mara nyingi, zaidi kibiashara. Mwaka 2010 sote tulibahatika kuingia bungeni. Tulijenga urafiki na kushirikiana mambo mengi. Tuliunganishwa na mambo mengi; upenzi wa @simbasctanzania, siasa, na ujasiriamali. Kwa mahusiano/historia hii haikuwa tabu kumwomba mkopo wa pikipiki, tena wa mwezi mmoja tu. Mimi kama mkulima/mfanyabiashara ya mazao, ninakuwa na ‘stock’ ambayo huuza bei zikichangamka. Na yeye si mgeni kwenye hili. Ndiyo biashara. Kwa kuwa yeye ni jamaa yangu, na ana stock ya pikipiki, kuniazima haliwezi kuwa jambo zito saaana, kama naweza kuweka dhamana. Wapiganaji mjini tunafanya sana hii. Kwa wale maskini wenzangu, kukopa ni upiganaji unaosaidia kufanikisha jambo na wala siyo jambo la aibu, kimsingi ni harakati ya kupambana na uma.
#sportskitaa #sportskitaa #sportskitaa #sportskitaa #sportskitaa #sportskitaa #talentonlineTv

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *