
UTULIVU WA KWELI UTALETWA NA MATOKEO TU naandika exaud_msaka_habari Utulivu wa uhakika kwa hizi timu mbili za kariakoo utalet…
UTULIVU WA KWELI UTALETWA NA MATOKEO TU
naandika exaud_msaka_habari
Utulivu wa uhakika kwa hizi timu mbili za kariakoo utaletwa na matokeo ya uwanjani
Umewahi kujiuliza ingekuwaje Simba kama ingekuwa haifanyi vizuri uwanjani
Umewahi kuwaza Simba ingekuwa inafungwa kila siku, haijafika mbali africa, haina mafaniko yanayoonekana, alafu yanatokeo haya yaliyotokea unadhani hali ingekuwaje?
Hivi unaanzaje kumwambia shabiki wa Simba kwamba kuna sintofahamu kwenye uwekezaji wakati timu yake inashinda uwanjani
Utaanzaje kuwaambia wanachama wa simba wamchukie muwekezaji wao wakati tangu ameingia wao wanacheka tu viwanjani
Inahitaji akili ya ziada sana ukitaka kuingiza neno la tofauti kwenye timu yoyote ambayo inafanya vizuri uwanjani
Leo nimekutana na comment moja mtandaoni mtu anasema hatutaki billion 20 tena kama tunapiga mtu saba, nikawaza hivi huyu utatumia mbinu gani kumgeuza fikra zake
Soka la dunia limebadilika sana na aina ya mashabiki nao wamebadilika, zamani mashabiki walikuwa nao wanakula ndani ya timu, yani ikiwekwa billion 20 na wao kuna mahali wanapata hela
Ila soka la sasa mashabiki wao wanataka ushindi na mafanikio ya timu tu, waone usajili mkali, wafike mbali kwenye michuano mikubwa wakifanikiwa hayo basi hata uwaambie unawaibia watakuambia iba tu hatuna shida
Lazima viongozi na waendesha soka wasome hizi tabia mpya za mashabiki wa kisasa
ALL IN ALL SABA NI NYINGI SANA JAMANI
,
Comments (0)