Posted By Posted On

-Klabu ya Yanga imetozwa faini ya laki tano (500,000) Kwa kosa la mashabiki wa klabu hiyo kuwapiga mawe na chupa waamuzi wa mche…

-Klabu ya Yanga imetozwa faini ya laki tano (500,000) Kwa kosa la mashabiki wa klabu hiyo kuwapiga mawe na chupa waamuzi wa mchezo wa ligi kuu Kati ya Biashara na Yanga wakati wakienda kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa karume Musoma. Yanga ilishinda Kwa goli moja kwa bila (1-0)

-Afisa mhamasishaji wa klabu ya Yanga Juma Antonio Nugaz ametozwa faini ya laki tano (500,000) Kwa kosa la kufanya mahojiano na vyombo vya habari ndani ya eneo la kuchezea na kusababisha kuchelewa Kwa mahojiano ya kikanuni ya makocha na manahodha wa timu za Gwambina na Yanga kwenye mchezo namba 86 uliochezwa Misungwi Mwanza.

-Kocha wa Mwadui FC Khalid Adam amefungiwa mechi mbili (2) kuiongoza klabu hiyo Kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na wadishi wa habari mara baada ya kumalizika Kwa mchezo wa ligi kuu Tanzania Kati ya Simba dhidi ya Mwadui mchezo uliisha Kwa Mwadui kufungwa magoli 5-0.

-Klabu ya Kagera Sugar imetozwa faini ya laki mbili (200,000) Kwa kosa la kuchelewa uwanjani kwenye mchezo Kati ya Kagera Sugar dhidi ya Mtibwa Sugar. Kagera ilifika Saa 6:51 mchana badala ya saa 6:30 mchana muda uliowekwa kikanuni Kwa mchezo unaoanza Saa 8:00 mchana.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *