Posted By Posted On

Yanga SC vs Namungo FC Follow @mawele_jr Mtihani wa kwanza na mgumu kwa kocha Hemed Morocco ambae hii ndio mechi yake ya kwanz…

Yanga SC vs Namungo FC

Follow @mawele_jr

Mtihani wa kwanza na mgumu kwa kocha Hemed Morocco ambae hii ndio mechi yake ya kwanza tangu kujiunga na wababe hao wa Kusini.

Amekabidhiwa timu kutoka kwa kocha Thierry Hitimana ambae kwa msimu huu hakuwa na mfululizo wa matokeo mazuri.

Yanga SC inaendelea kuimarika siku baada ya siku chini ya Cedric Kaze, yes! hawana safu nzuri ya ushambuliaji lakini timu yao inafunga magoli kutoka katika kila kona ya uwanja.

Wana safu ya ulinzi ambayo imekuwa ngumu sana kufunguka na wana uwezo wa kucheza mipira ya aina tofauti.

Wazuri katika mipira ya juu na chini, kiufupi ndio safu bora zaidi ya ulinzi mpaka sasa katika ligi yetu wakiwa wameruhusu magoli 3 katika mechi 10 walizoshuka dimbani.

Namungo FC imekuwa ni ngumu sana kuitabiri inapokwenda kucheza na hizi timu kubwa bila ya kujalisha mfululizo wao wa matokeo uko katika hali gani.

Katika msimu uliopita hizi ni timu ambazo ziligawana alama katika michezo yote miwili, natarajia kuushuhudia mchezo wa ushindani katika dakika zote 90.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *