Posted By Posted On

Photos from YuzoSports’s post

Nyota wa mieleka, Undertaker amethibitisha rasmi kustaafu WWE baada ya miaka 30.

Undertaker, aliingia ulingoni katika mchezo wake wa mwisho wa Survivor Series Jumapili usiku, ambapo aliuhutubia umma wa mashabiki wa WWE Universe kwa mara ya mwisho ambapo Undertaker ambaye jina lake halisi ni Mark Calaway, alieleza ni kwanini ameamua kustaafu.

“Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara. Sasa muda wangu umefika. Muda wangu umefika wa kumuacha Undertaker apumzike kwa amani.”

Undertaker anastaafu akiwa ndiye mchezaji bora wa WWE kuwahi kushuhudiwa katika mashindano hayo na amekuwa ulingoni kwa miongo mitatu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *