Posted By Posted On

ZIFAHAMU SHERIA 17 ZA MPIRA WA MIGUU…..No 2✍️ . . – Mchezaji atakuwa ameotea Iwapo mpira Utapigwa golini Ukagonga mlingoti moj…

ZIFAHAMU SHERIA 17 ZA MPIRA WA MIGUU…..No 2✍️
.
.
– Mchezaji atakuwa ameotea Iwapo mpira Utapigwa golini Ukagonga mlingoti mojawapo Wa goli au mlinda mlango na kurudi ndani ya Uwanja na kuguswa na mchezaji aliyekuwa katika nafasi ya Kuotea .

_Aidha , Hakutakuwa na dhana ya kuotea pale mchezaji atakapokutana na mpira Uliochezwa na mlinda mlango .

–Mpira Wa kurushwa Hauna kuotea , Pia mchezaji hatakuwa ameotea endapo atapokea mpira katika eneo lake kabla hajavuka Mstari Wa katikati ya Uwanja .

12. MAKOSA YA UTOVU WA NIDHAMU

Ni kutenda jambo ambalo lililo nje ya kanuni za kimchezo Wa mpira Wa miguu au kuonyesha tukio lisilo la Kiungwana pale mchezaji anapokuwa nje au ndani ya Uwanja

Makosa atendayo mchezaji anaweza kuonywa kwa kadi ya Njano au Nyekundu na kutolewa nje ya Uwanja . kwa kawaida makosa yanayoonywa kwa kadi ya manjano ni kama Vile kushika na Kuunawa mpira bila kukusudia , Kumsukuma mchezaji Wa timu pinzani katika hali ya kutaka kuchukua mpira , Kupoteza muda , Kumvuta au kumshika mchezaji Wa timu pinzani wakiwa katika hali ya kucheza mpira

Makosa ya kadi nyekundu ni kama vile , Kutukana , Kupigana , Kucheza rafu kwa nyuma , Kukaba kwa nguvu kwa kunyoosha miguu mmoja au yote miwili mbele wakati mchezaji mwingine anataka kupokea mpira au kucheza N.K

Kwa mujibu Wa sheria hii

–Mchezaji atakayeonyeshwa kadivnyekundu ya moja kwa moja atakosa mechi 3

–Mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano 2 katika mchezo mmoja atatolewa kwa kadi nyekundu na kukosa mchezo 1

–Mchezaji akionyeshwa kadi za njano katika michezo 5 ndani la Ligi 1 au mashindano atakosa mechi 1 , kadi 10 atakosa michezo 2 na kadi 15 atakosa michezo 3

–Endapo mchezaji atafikisha kadi za njano 20 katika msimu mmoja , basi kamati ya maadili ya wachezaji itakaa na kuamua adhabu kwa mchezaji huyo

13. PIGO HURU

Ni hali ya mwamuzi Wa michezo kuamuru mpira upigwe kuelekea upande Wa timu ya mtenda makosa

–Wakati mpira Unapigwa golini , Wachezaji wengine wanatakiwa kuwa katika Umbali Usiopungua mita 9.15 au hatua zisizopungua 10 kutoka pale mpira Ulipo.

14 . PIGO LA PENATI

Ni kitendo cha mpira kutengwa kwenye Kisanduku cha meta 12 kutoka goli .Pigo la penati linawahusisha wachezaji wawili tu , mpigaji na mlinda mlango na wachezaji wengine wrote wanatakiwa kuwa nje ya 18

Kuna aina 2 za pigo la penati ambazo ni , Penati ndani ya muda Wa mchezo yaani ndani ya dk 90′ na pigo la penati baada ya muda Wa mchezo ambalo linalenga kutafuta mshindi Wa mchezo Mara baada ya timu zote kutoshana nguvu ndani ya dakika za mchezo.

Mpiga penati ndani ya muda Wa mchezo hufanya mambo mawili ambayo ni Kupiga mpira golini 1 kwa 1 au kumtengea mwenzake aliye nje ya 18 ….mfano mzuri ni Lionel messi na Luis Suarez msimu Wa 2015/2016

–Mpigaji Wa penati anaruhusiwa kuucheza tena mpira uliorudi ndani ya Uwanja baada ya mlinda mlango kuucheza na hatoruhusiwa kuucheza endaoo Utagonga mlingoti na kurudi Uwanjani

15. MPIRA WA KURUSHA

Hutokea pale ambapo timu pinzani watakapokuwa wameutoa .

Hauhusiani na GoaL Kick , na Utarushwa kuelekea katika Lango la aliyeutoa

16 . PIGO LA GOLI

Hiii ni GoaL Kiki , Hutokea endapo timu shambulizi ikatoa au kupaisha Juu au pembeni ya Lango shambuliwa

17. PIGO LA KONA

Baada ya timu shambuliwa kutoa katika Mstari Wa goli alishi , timu shambulia hupewa nafasi ya Kupiga Pigo la kona katika timu pinzani ( shambuliwa ) .

Katika upigaji Wa kona mchezaji anaweza kupiga moja kwa moja au kuanza kwa Kupasia

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *